Na mwandishi wetu
Kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutajwa leo katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam kwa ajili ya maelekezo maalumu kuhusu usikilizwaji wake.
Katika hatua hiyo, pande zote zinatarajiwa kuwasilisha hoja zitakazobishaniwa mahakamani kutokana na madai yaliyowasilishwa kwenye kesi hiyo. Hoja hizo zitaiongoza mahakama kuamua idadi ya mashahidi wa kila upande na muda utakaotumika kusikiliza shauri hilo.
Kesi hiyo, ambayo ni ya madai ya mwaka 2025, ilifunguliwa na na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohamed, pamoja na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Bodi ya Wadhamini wa Chadema waliosajiliwa pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho. Shauri hilo linasikilizwa mbele ya Jaji Hamidu Mwanga.
0 Comments