Header Ads Widget

JACKSON KISWAGA AONGOZA KURA ZA MAONI ZA CCM JIMBO LA KALENGA



Mgombea wa nafasi ya Ubunge jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga ambaye pia ni mbunge  aliepita katika jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameongeza kwa kura za maoni katika jimbo la Kalenga.

Akitaja matokeo ya kura hizo Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sure Mwasanguti amesema kuwa Idadi ya kura zilizopigwa ni 8012 kura zilizoharibika ni 103 Idadi ya kura halali ni 1096 huku akimtaja Jackson Kiswaga kuongoza kura hizo.

“Matokeo ya kura za maoni kwa nafasi za ubunge  Jimbo la Kalenga ni kama ifuatavyo Henry Nyaulingo (304) Musa Mdede (1281) Grace Tendega ( 2391 ) Jackson Kiswaga (4036)”.

Aidha kufuatia matokeo hayo Matukio Daima Media  ilipata nafasi ya kuweza kuzungumza na Jackson Kiswaga mara baaada ya kutoka katika ofisi za CCM Wilaya ya Iringa kuchua matokeo katika ofisi hizo.

“Kwanza nichukue nafasi hii kukishukuru Chama changu kwa kuona nafaa kuweza kurudi tena katika nafasi hii  lakini pia niwashukuru wananchi wa Jimbo la Kalenga haswa wajumbe walioshiri kuweza kupiga kura na kuona  nafaa tena kuweza kupeperusha bendera ya chama changu na hii kwangu mimi ni ishara nzuri ya kwamba Chama changu bado kinaniamini na kama kitaona vema mimi kuongoza tena basi itakuwa ni jambo nzuri  ukizingatia jimbo la Kalenga halina historia ya kutawaliwa mara mbili”.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI