Header Ads Widget

EWURA YATOA ELIMU YA FURSA ZA NISHATI KWA WANANCHI WA KANDA YA ZIWA MAONESHO YA NANENANE


Na chausiku said

Matukio Daima, Mwanza

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa imetumia Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nyamhongolo, jijini Mwanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa zinazopatikana katika sekta ya nishati na maji.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 3, 2025, Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Muhina alisema mamlaka hiyo imejikita katika kutoa elimu ya ushiriki wa wananchi katika miradi mikubwa ya kimkakati, hususan mradi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) unaopitia mikoa ya Kagera na Geita.


 “Mtu yeyote anayetaka kushiriki katika fursa za mradi huu lazima apitie EWURA ili ajaze taarifa zake katika kanzidata yetu. Tupo hapa kuwaelimisha wananchi hususani wa vijijini wasiache kushiriki,” alisema Muhina.


Aidha, EWURA imetumia nafasi hiyo kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia sambamba na kufikisha ujumbe wa sera ya kitaifa inayolenga kufikisha asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.

 “Sisi kama wasimamizi wa eneo la gesi, tupo hapa kutoa elimu kuhusu matumizi salama na sahihi ya nishati safi kwa afya na mazingira bora,” aliongeza.


Katika nyanja ya uwekezaji, Muhina alisema EWURA sasa imerahisisha masharti ya kuwekeza kwenye vituo vya mafuta vijijini, hali inayowezesha hata watu wa kipato cha kati kuwekeza kwa mtaji wa kuanzia milioni 50.

 “Mpaka sasa tuna vituo vya mafuta 515 nchi nzima, kutoka vituo 270 vilivyokuwepo kabla ya Rais Dkt. Samia Suluhu kuingia madarakani. Wananchi wa Mwanza watumie fursa hii kuwekeza,” alisema.


Vilevile, EWURA imetoa wito kwa wananchi kufika katika banda lao kupata elimu kuhusu

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI