Header Ads Widget

DOGO JANJA AIBUKA MSHINDI KURA ZA MAONI NGARENARO, AWABWAGA WAKONGWE


Na,Jusline Marco;Arusha

Abdulazizi Abubakari Chende maarufu kama Dogo Janja, Mwanasiasa wa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi amechaguliwa na Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

Katika kura za maoni zilizofanyika leo Jumatatu Agosti 04, 2025, kulingana na wasimamizi wa uchaguzi Saphia Islam na Rajab Mwaliko, Dogo Janja ameibuka na ushindi wa Kura 76, akimbwaga Diwani aliyemaliza muda wake Bw. Isaya Doita aliyeambulia jumla ya kura 60 huku mshindi wa tatu akiwa ni Benjamin Mboyo aliyepata kura 2.

Dogo Janja anasifika kwa kuitetea na kuisema Kata ya Ngarenaro kupitia majukwaa mbalimbali ya kisiasa na burudani kupitia kazi zake mbalimbali za sanaa.

Wakati wa Kampeni zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi akiwa na Kaulimbiu isemayo "Nguvu ya Kijana, maendeleo ya Ngarenaro", Mwanasiasa huyo kijana ameahidi kujenga Ngarenaro mpya yenye mshikamano, maendeleo na yenye kuzingatia sauti na maamuzi ya wananchi, akiahidi kutumia nguvu, utashi na maarifa aliyonayo katika kuwaletea maendeleo wananchi wenzake wa Kata hiyo, Miongoni mwa Kata zinazounda Jiji la Arusha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI