Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma
MGOMBE wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 27 Agosti 2027, ameongoza msafara wa chama hicho kuelekea makao makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yaliyopo Ndejengwa, jijini Dodoma, kwa ajili ya kurejesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt. Samia amefuatana na mgombea mwenza wake Dkt. Emmanuel Nchimbi, pamoja na viongozi mbalimbali wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Alhaj Adamu Kimbisa. Walifika katika ofisi za tume hiyo majira ya saa 1:50 asubuhi, ambapo walipokelewa rasmi na Mkurugenzi wa INEC, Bw. Kailima Ramadhan.
Zoezi hilo linakuja baada ya Dkt. Samia kuchukua fomu ya kugombea tarehe 9 Agosti 2027, ikiwa ni sehemu ya mchakato rasmi wa uchaguzi unaosimamiwa na INEC.
Hadi sasa, vyama 17 vingine vimeshachukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya juu serikalini. Vyama hivyo ni pamoja na: NRA, AAFP, Chama Makini, NLD, UPDP, ADA-TADEA, UMD, TLP, CCK, CHAUUMA, DP, SAU, CUF, ADC, UDP, NCCR-Mageuzi, pamoja na ACT-Wazalendo.
0 Comments