Header Ads Widget

CCM YAZINDUA KAMPENI MWANZA, NCHIMBI ATAJA VIPAUMBELE SABA

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA 

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Emmanuel Nchimbi, leo Ijumaa Agosti 29, 2025, amezindua rasmi kampeni za chama hicho Mkoani Mwanza na kueleza mambo saba makuu yatakayotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela, ambapo mamia ya wananchi walihudhuria kushuhudia mkutano huo wa hadhara.

Amesema kuwa katika miaka mitano ijayo serikali itaboresha uwanja wa ndege wa Mwanza ili uwe na hadhi ya kitaifa, sambamba na kukamilisha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka pamoja na ujenzi wa meli mbili mpya katika Ziwa Victoria.


Aidha, amebainisha kuwa miradi mipya 76 ya maji itaanzishwa ili kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu inapatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa wananchi wa Mkoa huo.

Kwa upande wa makazi, Nchimbi amesema serikali itajenga nyumba za gharama nafuu zitakazopangishwa kwa wananchi, hatua ambayo inalenga kupunguza gharama za maisha na kuwaondolea wananchi mzigo mkubwa wa kodi za nyumba.

Vilevile, amesema serikali itarasimisha shughuli ndogondogo za wafanyabiashara ili kuwasaidia kupata mikopo kwa urahisi na hivyo kuongeza mitaji ya biashara zao na kukuza uchumi wa kaya.

Ameongeza kuwa serikali itaboresha sekta ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba katika Ziwa Victoria, hatua itakayoongeza ajira kwa vijana na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Mkoa wa Mwanza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI