Header Ads Widget

BARABARA YA MLIMBA MASAGATI KIPAUMBELE CHA MAENDELEO" DKT. RWAKATALE, AWASISITIZIA WANANCHI KUMUUNGA MKONO DKT. SAMIA

 


NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO 

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mlimba kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Rose Rwakatale, amesema wananchi wa Mlimba wanakabiliwa na changamoto kubwa ya barabara ya Mlimba hadi Masagati, changamoto ambayo ikitatuliwa itafungua fursa nyingi za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza mjini Morogoro wakati wa mkutano wa kampeni ya kuomba kura kwa mgombea urais na Mwenyekiti wa CCM Dkt. Rwakatale amesema barabara hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wanaotegemea kuuza mazao yao ndani na nje ya jimbo.

Alisisitiza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kutasaidia kuongeza tija katika kilimo, kupunguza gharama za usafirishaji na kufungua njia mpya za ajira na uwekezaji.

 Aidha amempongeza  Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa serikali yake imefanya mambo makubwa katika Jimbo la Mlimba na nchi kwa ujumla.

 Amesema mafanikio yaliyopatikana katika sekta za elimu, maji, afya, Nishati na mawasiliano ni ushahidi tosha wa dhamira ya kweli ya CCM kuwaletea Watanzania maendeleo ya haraka na ya uhakika.

“Jimbo la Mlimba limeona mabadiliko makubwa kupitia uongozi wa CCM. Huduma za maji safi na salama zimeboreshwa, sekta ya afya imeimarika, shule zimeongezwa na vijana wengi sasa wana nafasi ya kupata elimu bora. Haya yote ni matokeo ya kazi nzuri ya Mwenyekiti wetu wa CCM na Mgombea Urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tunapaswa kumuunga mkono kwa kumpa kura nyingi ili aendelee kutuletea maendeleo zaidi,” amesema Dkt. Rwakatale.

Dkt. Rwakatale aliwaomba wananchi wa Mlimba kuendelea kuiamini CCM, akisisitiza kuwa kura kwa Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kura kwa wagombea ubunge na madiwani wa CCM ndizo zitakazohakikisha jimbo hilo na Tanzania kwa ujumla vinaendelea kusonga mbele.

“Wananchi wenzangu wa Mlimba, tusikubali kurudishwa nyuma. Tuchague maendeleo, tuchague chama kinachotekeleza ahadi zake. Tumpigie kura Mwenyekiti wetu wa CCM na Mgombea Urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani kupitia CCM, ili tuwe na nguvu ya pamoja kuendeleza kazi kubwa iliyokwisha kuanzishwa,” alisisitiza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI