Header Ads Widget

CCM MKOANI MWANZA KUZINDUA KAMPENI AGOSTI 29.

 

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Omary Mtuwa, amesema chama hicho kitaifanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za chama hicho kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025 wa kuwachagua Rais, Makamu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Agosti 27, Mtuwa amesema Mkoa wa Mwanza umepata bahati ya kuwa Mkoa wa pili kuandaa kampeni, ambapo Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais ndiye atakayezindua kampeni hizo katika Mkoa huo, zitakazofanyika tarehe 29 mwezi huu katika viwanja vya Furahisha.

 “Sisi kama Chama Cha Mapinduzi tumejiandaa vizuri kushiriki kampeni katika Mkoa wetu wa Mwanza. Vipaumbele tulivyonavyo katika utekelezaji wa Ilani ya chama chetu vyote viko katika Ilani ya Uchaguzi, ambapo Mheshimiwa Mgombea Mwenza na wananchi watarajie kampeni zitakazofanyika Mwanza kuwa za kistaarabu, kampeni za mfano, zitakazonadi sera na kueleza serikali yake itafanya nini katika kipindi cha miaka mitano,” alisema Mtuwa.

Mtuwa alisema CCM Mkoa wa Mwanza imejiandaa vizuri kushiriki kampeni hizo ambazo zitakuwa za kistaarabu, za mfano, na zitakazonadi sera pamoja na kueleza wananchi nini serikali itafanya kwa miaka mitano ijayo kupitia Ilani ya Uchaguzi.

Vilevile aliwataka wanachama waliogombea nafasi mbalimbali lakini hawakufanikiwa katika kura za maoni kuungana, akibainisha kuwa kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama makundi yalishaisha tarehe 22 baada ya uteuzi wa wagombea wa ubunge na udiwani.

 “Sasa ni kundi moja la Chama Cha Mapinduzi. Tuungane kuhakikisha chama chetu kimeshinda,” alisisitiza.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa kampeni hizo, pamoja na wanachama wa CCM waliogombea nafasi mbalimbali lakini hawakupata ushindi kwenye kura za maoni.

“Ninaomba na ninawatka kwa mujibu wa katiba na kanuni zetu, makundi yalishaisha tokea tarehe 22 baada ya uteuzi wa wagombea wa Ubunge na Udiwani. Sasa ni kundi moja la Chama Cha Mapinduzi. Tuungane kuhakikisha chama chetu kimeshinda,” alisisitiza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI