Header Ads Widget

BUTEMBO ACHUKUA FOMU YA UDIWANI KWA KISHINDO KATA YA MAGOMENI DAR




Na. Mwandishi Wetu Dar.

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Magomeni iliyopo Manispaa ya Kinondoni kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Noordin Yusuph Hassan 'Butembo' leo Agosti 17, 2025 amechukua fomu rasmi  kwa Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata tayari kwa kinyang'anyiro cha uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Butembo amekabidhiwa fomu hiyo na Afisa Mtendaji Bi. Emmaculate Katto kwa niaba ya Mtendaji wa Kata hiyo ambapo ametakiwa kuipitia na kisha kuijaza na kuirejesha ndani ya siku tatu.

Hata hivyo, baada ya kupokea fomu hiyo, Butembo ameahidi kuijaza na kisha kuirejesha Agosti 19, 2025.

"Nashukuru Chama chetu kwa hatua zote za mchakato wa uteuzi na kisha kunirejesha kwa hatua hii ya sasa.

Nipo mguu sawa kufanya kampeni za ustaarabu na kishindo kuhakikisha ushindi wangu wa Udiwani na ushindi wa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge kwa Jimbo la Kinondoni.

Lakini pia niwashukuru viongozi wa CCM Kata ya Magomeni katika hatua zote na sasa tunaenda kukipigania Chama nje kwa Wananchi, tuendelee kushikamana kwa pamoja " amesema Butembo.





Aidha, Butembo amewaomba Wana CCM wa Kata hiyo pamoja na Wananchi kujitokeza kwa wingi Agosti 19, 2025 kwa shangwe wakati wa kuirejesha fomu hiyo.

"Shangwe hizi tutakuwa nazo tena Jumanne Agosti 19, 2025 kuanzia saa Nane mchana kwa umoja wetu huu huu nitakaporejesha fomu" Amesema Butembo.

Butembo ni kada wa CCM amekuwa Diwani wa Kata ya Magomeni kuanzia 2020-2025, na sasa anapeperusha tena bendera ya CCM kwa awamu ya pili.

Miongoni mwa mambo makubwa aliyofanya ndani ya Kata hiyo ni pamoja na kusimamia masuala ya Msingi ikiwemo Elimu, Afya, Mazingira na miundombinu pamoja na mikopo nafuu kwa makundi maalum inayotolewa na Manispaa ya Kinondoni.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI