Header Ads Widget

BREAKINGNEWS:AJALI BASI LA IBABA MUDA HUU

 


Abiria zaidi ya 50 waliokuwa wakisafiri na basi la Ibaba lenye namba za usajili T 408DQC Kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam wamepata ajali eneo la Chamakweza kabla ya kufika Vigwaza mkoa wa Pwani. 

Ajali hiyo imetokea saa 3:20 usiku huu leo Alhamis Agosti 28/2025 imesababishwa na lori lililokuwa likitaka kulipita gari jingine mbele na kutaka kugongana  uso kwa uso na basi hilo kabla dereva wa basi kulitoa basi hilo nje ya barabara na kupelekea kupasuka taili la  mbele upande wa dereva. 

TAZAMA FULL VIDEO YA AJALI BOFYA LINK HII


Hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya majeruhi mwandishi wa matukio Daima Media Francis Godwin ni mmoja wa abiria waliokuwepo kwenye ajali hiyo Ila amesema ametoka salama anamshukuru Mungu. 



Godwin alisema dereva wa basi hilo amefanya jitihada kubwa kuepusha madhara makubwa kwani nje ya hapo madhara makubwa zaidi yangetokea. 













Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI