Header Ads Widget

ALIYEKATWA UBUNGE TARIME MJINI AWATAKA WAJUMBE KUWA WATULIVU


Na Hamida Ramadhan, MatukuoDaima Media Dodoma 

WANANCHI  wa Tarime Mjini wametakiwa kuwa watulivu na kuendelea kuwa na mshikamano, kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliolenga kumpata mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao.

Kauli hiyo imetolewa leo, Agousti 25 ,2025 jijini Dodoma na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Michael Kembaki ,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatima ya mchakato wa kura za maoni na mwelekeo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Kembaki, ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitano bungeni, amewashukuru wananchi wa Tarime kwa ushirikiano waliompa wakati wa uongozi wake, pamoja na wajumbe waliompa kura katika kura za maoni. Katika mchakato huo, Kembaki alipata kura ,5572, 

Hata hivyo, anasema kuwa chama kilifanya maamuzi yake kupitia ngazi mbalimbali  kuanzia vikao vya kata, wilaya, mkoa hadi taifa  na hatimaye kumpitisha mgombea mwingine kupeperusha bendera ya CCM.

"Uongozi ni kupokezana," Katika kipindi hiki chama kimefanya maamuzi Mimi niko tayari kushirikiana kwa hali na mali na yule aliyepitishwa ili kuhakikisha ushindi wa CCM unapatikana,"Kembaki

Aidha, Kembaki amewapongeza wananchi wa Tarime Mjini kwa kuwa sehemu ya mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake na kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kipindi cha miaka mitano, sambamba na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa miradi mingi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa zaidi ya asilimia 80 katika jimbo hilo.

“Nawaomba wana CCM wenzangu, huu si wakati wa makundi. Kama kulikuwa na makundi wakati wa mchakato, basi yabaki kuwa historia sasa ni wakati wa kuwa na kauli moja na mshikamano wa dhati ili kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo,” amesisitiza.

Amewasihi wananchi wote, bila kujali nani walimuunga mkono awali, waungane sasa kumuunga mkono mgombea aliyeteuliwa rasmi na chama.

 “Msimamo wangu ni kuhakikisha tunampa kura za kutosha aliyeteuliwa hali hii imeshatokea, sasa tuwe wamoja nawaomba kwa moyo wa dhati, tuendelee kushikamana,”


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI