Header Ads Widget

AFISA MWANDAMIZI AHUKUMIWA MIAKA MINANE JELA KWA UBADHIRIFU

 

Na mwandishi wetu

Mahakama nchini Guinea ya Ikweta imemhukumu kifungo cha miaka minane jela aliyekuwa Afisa mwandamizi wa serikali, Baltasar Ebang Engonga,baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, Engonga alipatikana na kosa la kujinufaisha binafsi kwa kutumia fedha za serikali, kinyume cha maadili ya utumishi wa umma. Mbali na kifungo hicho, ameamriwa kulipa faini ya dola 220,000 kama fidia kwa hasara aliyosababisha kwa taifa.

Shauri hilo liliibua mjadala mkubwa mwaka jana baada ya uchunguzi wa vyombo vya usalama kubaini matumizi mabaya ya fedha na kupatikana kwa mamia ya video za ngono kwenye vifaa vya kielektroniki vya Engonga. Video hizo, ambazo zilivuja kwenye mitandao ya kijamii, zilihusishwa na safari na vikao vya kifahari vilivyogharimiwa na fedha za umma.

Hukumu hii imechukuliwa kuwa ishara ya mabadiliko katika msimamo wa serikali ya Guinea ya Ikweta kupambana na vitendo vya rushwa na utovu wa maadili miongoni mwa viongozi wa umma. Hata hivyo, wachambuzi wanasema kuna mashaka iwapo hatua hiyo ni ya kipekee au sehemu ya mageuzi makubwa ya kiutawala.

Kwa sasa, Engonga anatarajiwa kuanza kutumikia kifungo chake huku taratibu za kisheria za kukusanya faini zikifuatwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI