Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amewasili jijini Kigali, Rwanda, kushiriki Mkutano wa 16 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda.
Mhe. Kombo amepokelewa na Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Bi. Isabelle Umugwaneza, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Kambanga, na maafisa wengine waandamizi kutoka pande zote mbili.
0 Comments