Header Ads Widget

WATOA HUDUMA YA AFYA SEKTA BINAFSI WAOMBWA KUDHIBITI UDANGANYIFU

 

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA

Watoa huduma wa afya kutoka sekta binafsi mkoani Mwanza wametakiwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kutoa taarifa za matumizi mabaya ya kadi za bima, ili kusaidia kuzuia vitendo vya udanganyifu vinavyoathiri huduma za afya kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Mwanza na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr, SilasWambura, wakati wa kikao kazi na wadau wa sekta binafsi kuhusu mabadiliko yanayoendelea kufanywa na mfuko huo, hususan katika eneo la kuchakata madai ya huduma za afya.

Wambura amesema kuwa kushindwa kutoa taarifa kuhusu matumizi yasiyo halali ya kadi za NHIF ni sawa na kuhujumu mfuko huo, ambao hutegemewa na wananchi wengi kupata huduma za matibabu kwa gharama nafuu.


Kwa upande wake, Meneja wa NHIF Mkoa wa Mwanza Jarlath Mushashu ameeleza kuwa sasa uchakataji wa madai unafanywa kwa kutumia akili mnemba (artificial intelligence), ili kuongeza ufanisi na kuondoa mzigo mkubwa wa kazi uliokuwa ukifanywa na binadamu.


Aidha, baadhi ya watoa huduma waliohudhuria kikao hicho wamekiri kuwa awali walikuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali, ikiwemo namna bora ya kujaza taarifa kwenye mfumo wa madai, lakini kupitia mafunzo hayo wamepata uelewa wa kutosha utakaowarahisishia kazi.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI