Header Ads Widget

SHILINGI BILION 1.5 KUWANUFAHISHA WAFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA KAGERA

 


Na Shemsa Mussa -Kagera

Kiasi cha Mkopo wa shilingi bilioni 1.5 umetolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwaajili ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na zana bora za uvuvi kwa wavuvi na wafugaji Mkoani Kagera.

Akizungumza katika mafunzo kwa wafugaji na wavuvi, Mkuu wa Mkoa Kagera Bi Hajjat Fatma Mwassa  amesisitiza kuzingatia elimu na mafunzo ya ufugaji wa samaki wanayopewa na wataalamu  huku akisema serikali imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya ufugaji huo wa njia ya vizimba na  lengo ikiwa ni wananchi  kujikomboa kimaisha,kutokomeza umaskini  na kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.


"Niwambie tu Serikali ya Awamu ya Sita imetoa mikopo ya shilingi milioni 10 kwa kila kizimba kwa ajili ya uendeshaji,na sisi kama mkoa yametengwa maeneo 12 yanayofaa kwaajili ya vizimba vya samaki na tayari vimba 52 vimesimikwa mpaka sasa" 

Wananchi zaidi ya 140 mkoani Kagera wamehudhuria mafunzo ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ili kuongeza uzalishaji wa samaki kutoka tani 32,349 zinazozalishwa kwa sasa,na  kuwa kizimba kimoja chenye ukubwa wa mita za mraba 256 kina uwezo wa kuzalisha tani 14 kwa muda wa miezi saba. 


Mafunzo ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba yanafanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera kwa siku mbili Julai 10 hadi 11, 2025 na yanaendeshwa na wataalam kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI