Header Ads Widget

WAGOMBEA UBUNGE SABA SAME MASHARIKI WAANZA KUPITA KUJINADI KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU .



NA WILLIUM PAUL, SAME. 


WAGOMBEA Ubunge saba jimbo la Same mashariki mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mbunge anayetetea nafasi yake, Anna Kilango Malecel wameanza safari ya kupita kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo kujitambulisha na kuomba kura. 


Wagombea hao ni pamoja na Miryam Mjema, Andrea Chezue, Adam Mzee, Dkt. Peter Kibacha, Nickson Mjema, na Daud Mambo ambapo zoezi la kujitambulisha na kuomba kura lilifanyika katika kata ya Vunta, Kirangare na Bwambo huku kila mgombea akinadi sera zake endapo atachaguliwa ataenda kufanya nini. 



Mbunge Anna Kilango, aliwaomba Wajumbe kumrudisha ili kwenda kumalizia kazi ambazo amekwisha zianza. 


Akiwa Vunta amewaeleza wananchi jinsi alivopambana kuileta serikali kuja kujionea jengo lililokuwa likiitwa Kituo cha afya hapo nyuma hali ambayo aliishawishi kuanza ujenzi mpya wa Kituo cha Afya ambao bado unaendelea. 



Mbunge huyo pia katika utawala wake ameweza kupambana kuhakikisha miundombinu ya barabara iliyokuwa katika hali mbaya inapitika hususani barabara ya Kidenge na kuwaomba Wajumbe kumda ridhaa ya kuongoza kipindi kingine aweze kumalizia ujenzi wa barabara hiyo mpaka kata ya Miamba. 


"Hakuna mtu ambaye amemaliza matatizo ya familia yake kwa siku moja natambua yapo mambo mengi nimeyafanya katika kipindi cha uongozi wangu lakini pia kunachangamoto chache bado hazijafanyiwa kazi nawaombeni nipeni tena miaka mitano nikamalizie kazi ambazo nimeshazianza msikubali tukarudi kule nyuma mwaka 2015 ambapo mlikosea kuchagua na kusababisha maendeleo kurudi nyuma" Alisema Anna Kilango. 



Naye Miryam Mjema aliahidi endapo atachaguliwa atahakikisha anawaunganisha wananchi wa Jimbo hilo ili kuleta maendeleo. 


Miryam alisema kuwa, zipo kero ambazo ni za muda mrefu ikiwemo ubovu wa barabara ambazo hazipitiki pamoja na uchakavu wa vituo vya Afya na shule na kuahidi endapo atachaguliwa atahakikisha anakarabati. 



Aidha mgombea huyo alizungumzia swala la Ugawaji wa halmashauri ya wilaya ya Same pamoja  na wilaya ili Jimbo hilo liweze kupata wilaya yake na kuahidi endapo atachaguliwa atahakikisha swala hilo linatekelezeka. 


"Maendeleo kwa sasa yanaenda kisayansi na teknolojia hata Ilani yetu ya uchaguzi 2025/2030 ipo kisayansi hivyo panapaswa kupatikana mtu sahihi wa kuongoza kisayansi na sio mwingine ni mimi nitumeni niwatumikie" Alisema Miryam. 



Naye Andrea Chezue alisema kuwa, yeye amefanya kazi kwa muda mrefu serikali katika nafasi mbalimbali hivyo anatambua jinsi ya kuishi na wananchi huku akiahidi kuhakikisha tatizo la ubovu wa barabara katika jimbo hilo linatatuliwa. 


Aidha aliahidi endapo atachaguliwa katika kipindi chake cha miaka mitano shule za sekondari zinajengewa mabweni ili kuhakikisha wanafunzi wanalala sehemu salama na ufaulu unaongezeka  pamoja na kuahidi kupambana kuhakikisha wilaya ya Same inagawanywa. 


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI