Header Ads Widget

WAFANYAKAZI WA NDEGE 180 WANAFUATILIA KULIPWA FIDIA BAADA YA KUGUNDULIWA KUWA NA SARATAN

 


Takriban wafanyakazi 180 wa sasa na wa zamani wa jeshi walio na saratani wanadai kuwa ilisababishwa na moshi wenye sumu kwenye helikopta na wanafuatilia Wizara ya Ulinzi ili kulipwa fidia.

Sajenti wa ndege wa RAF Zach Stubbings, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 47 mwezi Januari, ni mmoja wa watu sita ambao walikuwa wamefikia suluhu nje ya mahakama kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ingawa haijakubali kuwajibika.

Kundi linalowakilisha wanajeshi wa zamani limehimiza Wizara ya Ulinzi kuchukua hatua haraka ili kuwalinda wale ambao bado wanahudumu na pia kuongeza ufahamu miongoni mwa wanajeshi wa zamani.

Wizara hiyo ilisema inaamini kwamba moshi unaotoka kwenye injini haukuwa na hatari kwa afya lakini inafuatilia suala hilo.

Wizara ya Afya ilithibitisha mnamo Februari kuwa inajaribu kubaini idadi ya watu ambao wamehudumu kama wafanyakazi wa ndege ambao wamegunduliwa na saratani na ilikuwa ikifanya majaribio ya moshi wa injini ya ndege.

Mawakili wa Hugh James waliambia BBC kuwa inafuatilia madai yanayohusiana na ndege nne za kijeshi - Sea King, Westland Wessex, Puma Wessex, Puma na CH-47 Chinook.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI