Ujenzi wa mtambo wa kuzalisha Hewa Tiba (Oxygen Plant) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba umefikia asilimia 95, hatua inayotarajiwa kuboresha utoaji kwa wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo.
Akizungumza na viongozi kutoka Wizara ya Afya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa waliotembelea mradi huo Joannes Muga kutoka Sigma Gas and Engineering inayotekeleza mradi huo alisema kazi kubwa tayari imekamilika, na kilichobaki ni hatua chache za ukamilishaji mradi huo muhimu.
“Tunatarajia mtambo huu utakamilika na kuanza kutumika ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti 2025,” alisema Mhandisi huyo.
Mradi huo unatarajiwa kusaidia kupunguza utegemezi wa Hewa Tiba kutoka nje ya hospitali na kuimarisha huduma kwa wagonjwa wanaohitaji oksijeni ya haraka.
0 Comments