Header Ads Widget

WATU WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI WAPORA WAVUVI KIGOMA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WATU wanaoaminika kuwa majambazi wamewavamia wavuvi wanaofanya shughuli zao katika mwambao wa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma na kuiba mashine nne za boti na vifaa vingine vilivyokuwa vikitumiwa kwenye shughuli za uvuvi na wavuvi.

Akisimulia tukio hilo Mmoja wa wavuvi anayefanya shughuli zake katika Mwalo wa Kibirizi manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, Mohamed Kassim alisema kuwa tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Nondwa kuelekea kijiji cha Mtanga Halmashauri ya wilaya Kigoma.


Mohamed alisema kuwa tukio hilo lililoanza majira ya saa nne usiku hadi saa 10 alfajiri ambapo wavuvi walijaribu kuwasiliana na polisi wanamaji lakini hakuna msaada wowote ambao uliweza kupatikana hadi majambazi hayo yalipomaliza kufanya uharamia wao hii ikiwa ni mara ya pili kwa tukio la ujambazi mkoani Kigoma tangu Mkuu mpya wa mkoa huo Simon Sirro kuripoti mkoani Kigoma.

 Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Filemon Makungu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa katika tukio hilo lililotokea kijiji cha Mtanga Kigoma Vijijini majambazi hayo  yalifanikiwa kuondoka na mshine nne za boti aina ya Yamaha,Betri 10 za solar N70, simu tano za mkononi na lita 240 za mafuta ya dizeli.


Kufuatia tukio hilo Kamanda Makungu alisema kuwa polisi waliendesha msako na kufanikiwa kuwakamata watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo kati ya watu saba ambao wanaaminika walishiriki kwenye tukio hilo la ujambazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI