Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Kagera.Serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi imetoa fedha kiasi cha shilingi bilion 4.6 Kwa awamu ya kwanza Kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa Kagera.
Ujenzi wa jengo la ofisi hiyo mpya ya mkuu wa Mkoa wa Kagera utajengwa kwa jumla ya gharama ya shilingi bilioni 9 kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ujenzi utagharimu shilingi bilioni 4.6 litakalojengwa na Mkandarasi M/s Skywards Construction Company Limited wa kutoka Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wananchi katika eneo la kagambo kata rwamishenye itakapojengwa ofisi hiyo mbele ya Mkandarasi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa kwasasa ni muhimu Mkoa wa Kagera kuwa na ofisi ya kisasa yenye vifaa vya kisasa vinavyoendana na sayansi na teknolojia ili kutoa huduma nzuri na zenye uhakika kwa wananchi.
Aidha,Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa ofisi ya mkuu wa Mkoa ya sasa imepitwa na wakati kwani ilijengwa zaidi ya miaka 60 liyopita na kusema kuwa eneo ilipo ofisi Kwa sasa kuna changamoto ya maji kujaa kutoka ziwa Victoria jambo ambalo linapelekea eneo hilo kuwa hatarishi kadri ya siku zinavyosogea kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ndugu Gozibert Kakiziba Mkurugenzi wa Kampuni ya M/s Goztecture (Mshauri Elekezi) wa mradi alisema katika hafla hiyo kuwa mchoro wa jengo jipya la ofisi ya mkuu wa mkoa umezingatia mambo muhimu manne ambayo ni Uimara wa jengo Uzuri wa jengo kuwavutia wananchi na wawekezaji, uoto wa asili kutunzwa ili mandhari kuvutia, mwisho jengo hilo litazingatia utawala au mamlaka kwenye usanifu wake,pia amemsisitiza Mkandarasi kufanya kazi yake kwa ufanisi na kuhakikisha anajenga kwa viwango kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Naye,Mhandisi Raphael G. Nyatega, Mhandisi kutoka ofisi ya Mkoa Kagera amesema faida za utekelezwaji wa mradi huo ni kuboresha utoaji wa huduma nzuri kwa wananchi, kuboresha utendaji kazi kwa watumishi, kuvutia wawekezaji kwa kuwa mkoa wa Kagera upo katika eneo la mpaka wa nchi jirani.
Naye Mkadarasi Bw Haamid Ashraf kutoka M/s Skywards Construction Company Limited ameeleza kuwa atahakikisha anakamilisha ujenzi wa jengo la ofisi hiyo kwa awamu ya kwanza kulingana na mkataba ndani ya miezi 12.
0 Comments