Header Ads Widget

MITAALA MIPYA 32 ILIYOZINDULIWA NI FURSA KWA WATANZANIA KUPATA ELIMU NA UJUZI.

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD kimezindua rasmi jumla ya mitaala Mipya ya 31 itakayotumika katika Udahili na Usajili wa mwaka wa masomo 2025/26.

Akizindua mitaala hiyo Julai 15 Mkuu wa Chuo hicho Dkt.Bakari George amesema Mitaala hiyo itatumika kidahili na kusajili wanafunzi wa ngazi ya cheti, Stashahada,Shahada za awali na Shahada za Uzamili kwa mwaka wa masomo 2025/26.

Aidha  amesema Taasisi ya Maendeleo ya Jamii imekuwa mstari wa mbele kubuni mitaala ambayo inahimiza fikra na ujuzi wa kutatua changamoto mbalimbali kwa wahitimu wake na kujibu changamoto ambazo zinaikabili jamii kwa sasa ambapo amesema mbali na kuanzisha program hizo mpya za mafunzo Taasisi hiyo itaendeleza jitihada kwa wahitimu ili waweze kuwa miongoni mwa wahitimu Bora wanaozalishwa na taasisi za elimu nchini.

Amesema Taasisi hiyo itaendeleza kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali kwa kutekeleza kwa vitendo sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 inayoelekeza Taasisi za elimu ya juu nchini kujenga uwezo wa wanataaluma ili waweze kutoa na kuendeleza maarifa mapya kupitia utafiti,machapisho yenye ubora na kutatua changamoto zinazoikabili jamii nzima ya watanzania.

Ameongeza kuwa Taasisi ulitaendelea kuweka mkazo kwa wanafunzi wake kujitolea maarifa na ujuzi kupitia kituo cha kimataifa huduma Tandaa na ubunifu wa kidujitali ili kuwajengea wanafunzi uwezo katika kukuza vipaji vya kibunifu.

Naye Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo hicho Bi. Janeth Zemba wakati akitoka neno la shukrani amesema Chuo hicho kimedhamiria kuendelea kuboresha mazingira kujifunza na ufundishaji ili kizalisha wataalam wenye weledi.

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Taaluma,Utafiti na Ushauri Elekezi Dkt. Juma Almasi Mhina amesema maandalizi ya mitaala hiyo yamezingatia maelekezo ya serikali,mahitaji halisi ya Jamii na mabadiliko ya kimataifa yanayohitaji wataalam waliobobea katika nyanja mbalimbali.

Ameongeza kuwa mitaala hiyo ni matokeo ya kazi ya pamoja baina ya wataalam wa ndani ya Taasisi na wadau wa nje kutoka sekta binafsi na Umma ambapo tathimini ya kina imefanyika ili kuhakikisha kuwa kozi hizo zinajibu vema mahitaji ya soko la ajira na kuchochea tafiti na uvumbuzi katika maeneo ya kijamii,kiuchumi, kutawala na kiteknolojia.

Ameongeza kuwa kupitia mitaala hiyo Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imelenga kuwa sehemu ya suluhusho kwa kutayarisha wataalamu wenye weledi,maadili na uwezo wa kubadilisha jamii kutoka kwenye changamoto mbalimbali ikewemo mabadiliko ya tabia nchi,mmomonyoko wa maadili,uongozi dhaifu ,ukosefu wa ajira pamoja na mapinduzi ya teknolojia.

Sambamba na hayo amewataka wahadhiri,walimu na wakufunzi kujiandaa vyema katika kusimamia itekelezaji wa mitaala hiyo ili kuwa Bora na yenye kustahili huku akiwataka viongozi wa Taasisi hiyo kuendelea kuweka mazingira Bora ya kujifunza na wanafunzi kujitokeza kwa wingi kunifaika na fursa hizo mpya.

Mitaala iliyozinduliwa ni pamoja na Shahada ya Uzamili katika maeneo ya Jinsi na haki za binadamu, Mabadiliko ya tabia nchi na jamii himilivu, Mabadiliko ya tabia nchi na Usimamizi wa mazingira, Shahada ya Kwanza katika maeneo ya Usimamizi wa rasilimali watu, Ustawi wa jamii, Uhasibu na Usimamizi wa Fedha  pamoja na Utawala na Usimamizi katika serikali za mitaa.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI