Header Ads Widget

MAANDALIZI YA HAFLA YA UZINDUZI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 (DIRA 2050),YAKAMILIKA,RAIS DKT SAMIA MGENI RASMI

  

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

NA MATUKIO DAIMA MEDIA DODOMA

MAANDALIZI  ya hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Dira 2050) yamekamilika ambapo uzinduzi wa Dira hiyo utafanyika tarehe 17 Julai 2025 huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .

Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Dkt. Fred Msemwa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Dkt. Fred Msemwa uzinduzi huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete, Dodoma.

Uzinduzi wa Dira 2050 unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wananchi 5,000 kutoka sehemu mbalimbli ndani na nchi ya nje. 

 Prof. Kitila Mkumbo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mpingo na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, katika taarifa iliyotolewa kwa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) hivi karibuni alisema kuwa maandalizi ya Dira 2050 yalishirikisha wadau mbalimbali waliotoa maoni yao kuhusu Tanzania wanayoitaka ifikapo mwaka 2050.

Prof. Kitila alisema maoni hayo ndiyo msingi wa Dira 2050 itakayozinduliwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Alhamisi ya tarehe 17 Julai 2025  jijini Dodoma.

Taarifa imetolewa na Dkt. Fred Msemwa.

KATIBU MTENDAJI TUME YA TAIFA YA  MIPANGO (NPC).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI