Header Ads Widget

TICD YA TUNUKU VYETI KWA WAHITIMU DURU YA KWANZA 2025

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Wahitimu sekta ya Maendeleo ya Jamii katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wametakiwa kutumia taaluma zao katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye jamii.


Akizungumza katika maafali ya 15 Duru ya Kwanza 2025 dirisha la Machi 2024/25 ikiwa ni maafali ya kwanza katikati ya mwaka ,Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George amewaambia wahitimu hao kuwa elimu hiyo ijawasaidie kuwa watu Bora na kuwaongezea tija kwenye utendaji kazi wao.


Awali akizungumza katika maafali hayo Naibu Mkuu wa Taasisi,Taaluma,Utafiti na Ushauri Elekezi Dkt. Almasi Juma Mhina mbali na kuwapongeza wahitimu hao amesema Taasisi hiyo inaendelea kutoa mafunzo kwa kuzingatia mfumo wa elimu ya mafunzo ya ufundi ambayo inawezesha mhitimu wa taasisi kupata ujuzi,maarifa na stadi maalum.

Aidha ameongeza kuwa taaisis hiyo pia imeendelea kutekeleza mpango mkakati wa miaka mitano 2023/24 hadi 2027/28 kwa kuendelea kuongeza zaidi program za mafunzo ambapo katika mwaka wa masomo 2025/26 Taasisi inakusudia kuanzisha jumla ya program mpya 16 za mafunzo sawa na asilimia 59 ya mitaala 27 iliyopo sasa na hivyo kufanya Taasisi kuwa na jumla ya programu za mafunzo ya muda mrefu 43.


Ameongeza kuwa mbali na program hizo Taasisi hiyo imeendelea kusimamia maelekezo ya serikali kuhusu kuwa kituo cha kitaifa cha kidigitali cha ubunifu ambapo mkazo umeendelea kuwekwa kupitia kituo cha huduma Tandaa na ubunifu wa kidigitali ili kuwajengea wanafunzi uwezo katika kukuza vipaji vya kibunifu huku zaidi ya asilimia 30 wanafunzi wahitimu wamepatiwa mafunzo hayo kupitia kituo hicho.


Dkt. Mhina ameongeza kuwa kituo hicho kinaendelea kuwashirikisha wanafunzi katika shughuli mbalimbali za ushirikishwaji jamii ili kubaini changamoto za fursa za maendeleo ambapo baadhi ya wanafunzi wameweza kuvifikia vijiji  na mitaa kushiriki mikutano ya wananchi na kusaidia kuibua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kitengeneza mipango ya kutatua changamoto hizo kwa kushirikiana na wataalamu wa maendeleo ya jamii kutoka Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru.


Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkuu wa Taasisi hiyo ,Mipango, Fedha na Utawala Bi.Janeth Isdory Zemba amesema Taasisi ya amaendeleo ya Jamii Tengeru itaendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli zake ikiwemo kuhakikisha wanafunzi wanahitimu kwa wakati na kutekeleza mpango mkakati wa miaka miaka mitano 2023/24 hadi 2027/28 kwa kuendelea kuongeza program za mafunzo.


Ameongeza kwa kuwata wahitimu hao kuwa wepesi katika kuangalia sehemu ambazo maarifa na ujuzi wao unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi kuliko kusubiri ajira kutoka serikalini au katika Taasisi binafsi.


Hata hivyo jumla ya wahitimu 174 wa ngazi za  shahada za uzamili,stadhahada ya uzamili, stashahada na Astashahada dirisha la Machi wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu yao hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI