TAASISI ya Elimu nchini (TET) imeendelea kutoa elimu kwa Umma juu ya matumizi sahihi ya Nukta nundu (BRAILLE) masomo wanayotumia Wanafunzi wenye uhitaji maalum wasioona.
Elimu hiyo wanaitoa katika banda lao ndani ya maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara (Saba Saba) ikiwa ni kuongeza uelewa kwa jamii.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mhakiki wa maandishi ya Nukta nundu (Braille) kutoka TET, Bi. Hadija Mahungu Salum amesema Jamii inahitaji kuelewa vitabu hivyo na Vifaa mbali mbali wanavyotumia wasioona na wale wenye uoni hafifu.
"Tunaonesha vitabu vya maandishi ya wasioona ambayo wanatumia Wanafunzi na Walimu wasioona pia.
Hii ni katika elimu ya awali, shule za Msingi na na Vyuo vya Walimu." Amesema.
Aidha, amebainisha kuwa, Katika mahitaji ya wasioona kuna matumizi ya fimbo, ubao wa kujifunza alfabeti, ubao wa namba.
"Mbali na breill pia TET tunaandaa vitabu vya maandishi yaliyokuzwa (large print) kwa ajili ya Wanafunzi wenye huoni hafifu hivyo Vifaa vyote vipo hapa na tunatoa elimu kwa watu wote.
Ukifika Banda letu la TET pia utaona Vifaa hivi ikiwemo Karatasi za michoro zipo za 'brelon' kwa ajili ya mchoro mguso kwa wasioona, lakini pia 'Stylus' ambayo ndo Kalamu ya kuandika kwa watu wasioona.
Aidha, ameishukuru Serikali kwa kufanikisha vitabu vya kutosha kwa hatua hii walengwa wamepata mahitaji ya kutosheleza kwa shule zote.
TET imechapisha vifaa na vitabu vya Kidato cha kwanza hadi sita vya Braille na Maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya mwanafunzi wenye mahitaji maalumu ya kutokuona na uoni hafifu nchini
Vitabu hivi vimechapwa katika uwiano wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja (3:1).
Vitabu, hivyo ni vya masomo ya Geography, Kiswahili, Civics, Agriculture, English, History, Biology, information and Computer Science na Mathematics.
Vitabu hivi vinamwezesha Wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya uoni kujifunza kama ilivyo kwa wanafunzi wengine na kupata stadi na mahiri mbalimbali zitakazowawezesha kumudu changamoto mbalimbali katika tendo la kujifunza.
Ambapo pia vimesambazwa katika shule 764 za wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu Tanzania Bara na Zanzibar.
0 Comments