Ripoti ya uchunguzi wa awali katika ajali ya ndege ya Air India 171 imetolewa.
Ripoti hiyo inasema injini zote mbili za ndege hiyo zilipoteza nguvu yake baada ya swichi mbili za kudhibiti mafuta kusogezwa kutoka sehemu zinapotakiwa kuwa hadi kwingineko jambo ambalo liligundulika na mmoja wa marubani muda mfupi baada ya ndege kupaa.
Rekodi za sauti kwenye chumba cha marubani, mmoja anasikika akimuuliza mwenzake "kwanini ulibadilisha swichi?" - mwingine anajibu, sikuzibadilisha.
Uchunguzi zaidi unaendelea na ripoti ya mwisho inatarajiwa kutolewa ndani ya mwaka mmoja, ripoti ya awali inasema.
Ripoti hiyo haimaanisha kufikia hitimisho ya kitu chochote badala yake imezua maswali mapya kuhusu swichi za kudhibiti mafuta na nini kilizifanya kubadilika katika sehemu zinapotakiwa kuwa.
Swichi zilirudishwa katika sehemu yake ya kawaida na kusababisha injini kuanza tena wakati imeshaanza kupaa.
Hadi wakati wa ajali hiyo, injini moja ilikuwa bado inarejesha msukumo wake wakati nyingine ilikuwa imesharejesha msukumo wake lakini bado haikuwa imerejesha nguvu yake kamili.
Ndege ya Air India 171 ilikuwa ya hewa chini ya sekunde 40 kabla ya kuanguka katika kitongoji kilichojaa watu katika mji wa magharibi mwa India wa Ahmedabad, na kuwa moja ya ajali mbaya zaidi ya anga nchini
Wanafamilia wa waathiriwa wanasema sababu ya ajali hiyo haitaondoa huzuni yao. "Bado tunakabiliana na hisia zetu kwa wakati huu, tukijaribu kukubali kilichotokea ," binamu wa mfanyakazi wa ndege hiyo
0 Comments