Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Saimon Siro ameitaka Halmashauri ya wilaya Kakonko mkoani Kigoma kutumia fursa ya kuwepo mpakani na nchii za Burundi na jirani ya Rwanda kuongeza uzalishaji wa mazao kuyafanya ya biashara ili kuinua uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo na nchi kwa jumla kutokana na soko la uhakika la mazao lililopo kwa nchi hizo.
Balozi Siro alisema hayo alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo ambapo alisema kuwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya kilimo utachochea maendeleo makubwa ya kiuchumi ya wananchi wa wilaya hiyo.
Alisema kuwa wilaya ina eneo kubwa linalofaa kwa kilimo ikiwa na rutuba ya kutosha na wananchi wanayo ari ya kufanya kilimo biashara hivyo Halmashauri inapaswa kuweka mipango ambayo itawaunganisha wananchi hao na fursa za kuongeza uzalishaji zinazoenda sambamba na fursa ya masoko.
0 Comments