MSANII wa Muziki wa kizazi kipya Barnaba Classic ametembelea banda la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na kupata maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo pamoja na kusaini kitabu cha wageni katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara SabaSaba, Julai 10,2025.
Katika banda hilo, Barnaba amepata kuelezewa shughuli za Sanaa ikiwemo kuzalisha Wasanii, viongozi wa Sanaa na Wafanyakazi katika Sekta ya utamaduni, sambamba na kuzalisha kazi za sanaa na huduma za Maltimedia.
Mbali na kutembelea Banda hilo, Barnaba pia ameweza kupanda jukwaa la SabaSaba na kutumbuiza Mashabiki waliojitokeza katika Kijiji cha Wizara ya Habari, Utamaduni na michezo.
![]() |
Msanii wa kizazi kipya, Barnaba Classic akisaini kitabu cha wageni Bandaa TaSUBa katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara (SabaSaba) Julai 10, 2025 |
Aidha, Barnaba amekuwa mdau mkubwa wa TaSUBa na ameweza kushiriki mara kwa mara shughuli za taasisi hiyo mjini Bagamoyo.
TaSUBa inatoa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) pamoja na Kozi za muda mfupi ( short course).
TASUBa ni Wakala wa Serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali, kifungu cha 245 kupitia tangazo la Serikali Na.220 la mwaka 2007 ikiwa na malengo ya kukuza,kuhifadhi na kutunza sanaa na Utamaduni wa Mtanzania ikiwa chini ya Wizara ya utamaduni, Sanaa na michezo.
0 Comments