Header Ads Widget

RC SIMIYU AAGIZA WANAOCHEZEA MIZANI YA PAMBA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.


MKUU wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha (wa pili kulia) akikagua mzani wa kununulia Pamba.


Na MATUKIO DAIMA, Meatu,


MKUU wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha  amewaagiza Wakuu wa Wilaya Mkoani humo kufanya  operesheni maalum ya kuwasaka na kuwakamata watu wanaochezea mizani janja za kupimia pamba na kuwaibia wakulima  na kuwafikisha mara moja katika vyombo vya kisheria.


Macha  ameagiza hayo  katika  ziara yake Wilayani Meatu baada ya  kupata taarifa za Wakulima wa zao la Pamba kuibiwa na  baadhi ya viongozi wa AMCOS wasio waaminifu.


Meneja wa wakala wa vipimo Mkoani Simiyu, Happy Titi amesema baada ya kufanya ukaguzi walibaini  mizani 91 kati ya  235 iliyokaguliwa  Wilayani Meatu imechezewa na  baadhi ya viongozi wa AMCOS kwa kushirikiana na Wataalamu wa mizani almaarufu vishoka.


Aidha ameeleza kuwa katika Wilaya zote Mkoani Simiyu jumla ya mizani 818 zilikaguliwa ambapo mizani 481 zimebainika kuchezewa na Viongozi wa AMCOS kwa kushirikiana na wataalamu wa mizani wasio rasmi almaarufu vishoka.


Mwisho. 










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI