NA MATUKIO DAIMA APP.
IRINGA.KUFUATIA ajali ya moto iliyotokea Mkoani Iringa na kuteketeza biashara za wafanyabiashara 335 katika soko la mashine tatu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote Mkoani hapo kuhakikisha katika masoko ya watu binafsi na serikali kunakuwa na mkakati maalumu wa ulinzi wa masoko.
RC Kheri James amesema hayo leo Julay 13,2025 wakati anazungumza na wahanga wa soko hilo na kubainisha kuwa mkakati huo utasaidia ulinzi wa mali zao, uhakika wa biashara na uendelevu na ukuaji wa biashara katika maeneo husika.
Alisema kumekuwa na changamoto ya ajali za moto na kuona masoko yanaungua katika maeneo mbalimbali na sababu za kuungua zikijirudia na kuelezwa kuwa ni changamoto ya miundombinu ya umeme, hujuma za kibiashara na uhalifu.
" Ukweli ni kwamba pamoja na changamoto nyingi za kuungua kwa masoko ni lazima kuimarisha mkakati wa ulinzi wa masoko,kwenye hili lazima kila soko liwe na kamati ya usalama ya soko"
Aidha alimuelekeza Kamanda wa Polisi wa Wilaya na Polisi kata ambao kata zao zina masoko kuwa watawajibika moja kwa moja kuwa sehemu ya usimamizi wa kamati hizo kuwa kuzijengea uwezo na kupojea taarifa za mara kwa mara juu ya mwenendo wa masoko husika.
" Mpeane mbinu za namna ya kudhibiti watu kuingia na kutoka,usalama wa soko waru wanapokuwa sokoni na wanapokuwa hawapo,panapoweza kuwekwa kampuni ua ulinzi pawekwe,ili panapotokea tatizo kampuni iweze kuwajibika,pale panapoweza kufungwa kamera pafungwe ili kujua muda huo nani aliinfia sokoni na kufanya nini"
Aliongeza kuwa " Kuwepo na watu ambao wanaweza kukagua wakati wa kufungua soko na kuona lipoje na wakati wa kufunga kutokana na wafanyabiashara wengine kuacha majiko yakiwaka na wengine kusahau kuzima gesi na baadae kutokea milipuko"alisema
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Jeshi la zimamoto na Tanesco kuweka utaratibu wa ukaguzi wa miundombinu ya masoko mara kwa mara na pale wanapobaini changamoto wanawajibu wa kuielekeza mamlaka zinazosimamia masoko husika kuchukua hatua ili wasiwe wanakutana kwa ajili ya majanga badala yake wakutane kwa ajili ya kudhibiti majanga.
"Niwaombe wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu mnachopitia changamoto ni nyingi,makwazo hayana budi kuja ila ole wake ayasababishayo Mungu atatuvusha hili nalo litapita, jambo la msingi ni kurudisha hali ya biashara, huduma na uchumi wa mtu mmoja mmoja" alisema
Awali akizungumza na wananchi hao alisema kuwa tayari hatua za uokoaji na uzimaji moto zimefanyika na kuweka usalama katika eneo hilo kinachofuata ni kuhakikisha biasharavzinarejea.
Alisema kuwa jukumu lao kama serikali ni kuhakikisha maadhimio yote, mipango ya muda mrefu na mfupi yaliyopitishwa na kamati ya maafa yanasimamiwa kwa ukamirifu.
" Tunafahamu wapo watu baada ya changamoto hii wamepotezabkila kitu na wapo baadhi baada ya hili wamenunua bidhaa zao kwa ajili ya kuuza,Yaliyotokea ni ajali kama ajali zingine msikubali kuchonganishwa na BAKWATA,viongozi wa soko wala kugombana ninyi kwa ninyi haya yametokea kama yanavyotokea katika maeneo mengine kikubwa tuache kazi ya aerikali kupitia zimamoto uchunguzi ukamilike na watareta taarifa ya uchunguzi"
MWISHO.
0 Comments