Header Ads Widget

IRAN IPIGE MARUFUKU MAKOMBORA YA MASAFA MAREFU IWAPO INATAKA MAKUBALIANO NA ISRAEL- NETANYAHU

 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel ametoa masharti ya kuunga mkono makubaliano na Iran, ikiwa ni pamoja na kuzuia mpango wa makombora wa Tehran.

Katika mahojiano  yaliyorekodiwa wiki iliyopita na kurushwa hewani jana usiku, Benjamin Netanyahu alisema anaunga mkono makubaliano "ya kipekee" na Iran ambayo yanajumuisha masharti matatu:

"Hakuna urutubishaji wa urani, kama Rais Trump na mimi tulivyosema... kupiga marufuku makombora ya balestiki ambayo yanaweza kuruka zaidi ya kilomita 482, ambayo ni kikomo kilichowekwa na makubaliano ya kimataifa ... na kuacha mhimili wa ugaidi..."

Haijulikani ni nini Bwana Netanyahu anamaanisha kuhusu "mikataba ya kimataifa ya vikwazo." Huenda anarejelea "Udhibiti wa Teknolojia ya Makombora," makubaliano ya kisiasa yasiyo rasmi kati ya nchi 35 yenye lengo la kuzuia kuenea kwa programu na teknolojia ya makombora.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi alisema jana: "Hatutafanya makubaliano yoyote ambayo hayajumuishi urutubishaji wa urani."

Ameongeza kuwa: "Iwapo kutakuwa na mazungumzo, mada itakuwa tu ya nyuklia na kujenga imani katika mpango wa nyuklia wa Iran kwa ili kuondolewa kwa vikwazo, na hakuna masuala mengine yatakuwa sehemu ya ajenda."

Maafisa wa Iran wamerudia kusema kwamba uwezo wa kijeshi na kiulinzi wa Iran hauwezi kujadiliwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI