Header Ads Widget

RAIS KUFANYA UZINDUZI RASMI WA BANDARI KAVU YA KWALA.

 


Na Mwandishi Wetu, Kibaha Matukio Daima Media

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya uzinduzi wa Bandari Kavu ya Kwala na safari za ubebaji wa mizigo kwa kutumia treni ya mwendokasi ya SGR kwenda Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alisema kuwa uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu Kwala Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.

Kunenge alisema kuwa Bandari Kavu ya Kwala ni kubwa na ya kisasa na itakuwa na uwezo wa kuhudumia makasha 823 kwa siku na makasha 300,000 kwa mwaka na kurahisisha usafirishaji na uchukuzi.

Aliongeza kuwa pia Rais ataweka jiwe la msingi kwenye Kongani ya viwanda hapa nchini iliyopo hapo Kwala ambapo kutajengwa viwanda 250 huku saba vikiwa vimeanza kazi na vitano viko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi.

Pia atahitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara kwa kuzungumza na wananchi wa mkoa wa Pwani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI