Header Ads Widget

'NCHI YA BURUNDI NI HURU,HAKUNA NCHI AU SHIRIKA LITAKALOKUJA KUIONGOZA NCHI YETU'- RAIS NDAYISHIMIYE

 

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye aliwakosoa Warundi wanaotafuta suluhisho la shida zao nje ya nchi.

Akizungumza katika maatdimisho ya miaka 63 tangu uhuru wa Burundi Jumanne, Ndayishimiye alisema: "Mrundi yeyote ambaye ana tatizo nchini na kwenda nje ya nchi kutafuta suluhisho, ni kwamba Mburundi huyo bado hajajifunza uhuru ni nini.

"Tunawaona kila wakati. Baadhi bado hawajui kuwa wanapelekwa nje ya nchi. Kwa hivyo ningependa kuwashauri wale Warundi. Ondoka kuzimu na uingie kwenye ubinadamu."

Aliwalinganisha na wanachama wa chama cha PDC (Wakati wa mapambano ya uhuru mnamo 1962, chama hiki kilifanya kampeni kutaka wazungu waendelee kuitawala Burundi).

Bila kufafanua zaidi, Rais Ndayishimiye aliwanyooshea kidole wale walioshindwa katika uchaguzi hivi karibuni wa bunge na manispaa, akisema mara moja waliugeukia Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kutafuta msaada.

"Kwa hivyo, Umoja wa Mataifa utawapigia kura? Wanaonyesha kwamba bado wana roho ya PDC," alisema.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wapinzani wa kisiasa wa serikali walioikimbia Burundi, waliungana katika makundi matatu: Cfor Arusha (Muungano wa Vikosi vya Upinzani vya Burundi kwa Kurejesha Mkataba wa Arusha), CN Inger ya Pfrage (Muungano wa Mwamko wa Taifa) na Map Burundi Buhire (Harakati za Kizalendo), walitangaza kuchukua hatua ya vita dhidi ya wizi wa kura uliofanyika hivi karibuni katika uchaguzi.

Mmoja wa wanasiasa hao Frederique Bamvuginyumvira, aliyekuwa Makamu wa rais, aliyewawakilisha wanasiasa amesema kuwa hawana chaguo jingine la kukataa matokeo ya uchaguzi zaidi ya kuchukua silaha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI