Mwandishi wa habari wa kujitegemea, Shomari Binda, amefariki dunia leo, Julai 3, 2025, kufuatia maradhi ya kisukari yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Mdogo wa marehemu, Omary Binda, amethibitisha taarifa hiyo kwa Matukio Daima Media na kusema kuwa hali ya Shomari Binda ilizidi kuwa mbaya siku ya jana ambapo walimkimbiza Hospitali madaktari wakasema damu yake imepungua kutokana na maradhi yake hali iliyosababisha umauti wake.
Marehemu Shomari Binda amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo Matukio Daima Media na vyombo vingine nchini yakiwemo magazeti mbali mbali kama Mtanzania na mengine.
Shughuli za mazishi ya mwanahabari Shomari Binda zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi, nyumbani kwao maeneo ya barabara ya Karume, mjini Musoma.
Matukio Daima Media tunatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanahabari wote walioguswa na msiba huu mzito.
Sisi sote ni wa mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
0 Comments