Mbunge
wa sasa wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu na aliyewahi kuwa mbunge
wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Simon Msigwa, wametajwa
miongoni mwa wagombea waliofanikiwa kupita katika mchujo wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Majina ya wagombea waliopitishwa
yametangazwa leo Julai 29, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
CCM anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, katika
mkutano uliofanyika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.
Mbali na Msambatavangu na Msigwa,
wagombea wengine waliopitishwa katika mchujo wa Jimbo la Iringa Mjini ni Moses
Ambindwile, Fadhili Ngajilo, Edward Chengula na Islam Huwel.
0 Comments