Header Ads Widget

MIMI NI YULE YULE SIJABADILIKA - BALOZI SIRO

 

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Siro amesema kuwa utendaji wake katika kusimamia masuala ya ulinzi na usalama haujabadilika hivyo  amewatahadharifa wananchi wa mkoa Kigoma kutojihusisha au kushirikiana na wahalifu kwani Kamanda Siro waliyekuwa wanamjua ni yule yule.

Balozi Siro ametoa maagizo hayo katika mikutano yake tofauti na watumishi wa umma akiwa kwenye ziara ya kiserikali mkoani Kigoma.

Siro ambaye  ni Ispekta Jenerali wa Polisi (IGP) Mstaafu alisema kuwa mapambano aliyokuwa anafanya kuzuia uhalifu na kupambana na majambazi akiwa Mkuu wa Operesheni na mafunzo wa Polisi na alipokuwa IGP  yataendelea Kigoma ambako yeye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa huo.

"Naujua Mkoa Kigoma vizuri nimetekeleza operesheni kimbunga kwa miezi sita najua kila kijiji cha mkoa huu na njia za wahalifu, haitakuwa kazi kwangu kujikumbusha na kusimamia mpango wa kudhibiti uhalifu mkoani Kigoma ,"Alisema Balozi Simon Siro.

Akiwa wilayani Buhigwe Mkuu wa wilaya hiyo, Michael  Ngayarina alisema wilaya imekuwa na Wimbi kubwa la raia wa Burundi wanaovuka mpaka na kuingia wilayani humo lakini vyombo vya ulinzi vimejipanga na kudhibiti matukio ya uhalifu lakini pia kusimamia ulinzi na usalama ili shughuli za uchumi ziweze kufanya bila matatizo.


Naye Mkuu wa wilaya Kasulu, Kanali Isack Mwakisu alisema kuwa wilaya hiyo ina idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji haramu wanaosababisha changamoto ya usalama lakini kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imefanya kazi kubwa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unasimamiwa vizuri.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI