Na Mariam Kagenda
Matukio Daima Kagera
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera wamehimizwa kuanzisha miradi yao Binafsi kupitia mishahara wanayoipata ili kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi .
Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatuma Mwassa amesema hayo wakati wa Tamasha la watumishi wa Halmashauri ya Missenyi ambalo liliambatana na michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba na Moira wa miguu likiwa na kauli mbiu isemayo "Mahusiano na afya bora kwa ustawi wa huduma bora kwa wananchi . Shiriki Uchaguzi mkuu Oktoba 2025
Hajjat Mwassa amesema kuwa si dhambi mtumishi wa umma kufanya shughuli za ujasiriamali ambazo zitamsaidia kujiongezea kipato kwani watumishi hao wanavyo vipawa mbalimbali hivyo Halmashauri itafute mashamba watumishi waweze kulima na kufuga Jambo ambalo litawasaidia kuongeza kipato.
Ameongeza kwa kuipongeza halmashauri hiyo kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuwa kazi kubwa imefanyika katika Halmashauri hiyo kwenye utekelezaji wa miradi ili kutatua changamoto ambazo wananchi walikuwa wakikabiliana nazo hasa uanzishwaji wa Mradi mkubwa wa ujenzi wa Soko la kisasa la kitega Uchumi Bunazi .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bwana John Paulo Wanga amesema kuwa lengo kubwa la Tamasha hilo ni kutafakari na kutathimini kwa kina yale yote mazuri yaliyofanyika katika awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania Doctor Samia Suruhu Hassani.
Amewahimiza watumishi wa Halmashauri hiyo kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo ili kuweza kutatua changamoto wanazokabiliana nazo wananchi huku akiwahimiza kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika Uchaguzi mkuu utakaofanyika October .
MWISHO.
0 Comments