Header Ads Widget

MAUAJI YA ALBERT OJWANG: NAIBU MKUU WA POLISI HAKUPATIKANA NA KOSA LOLOTE

 

Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi wa Kenya Eliud Lagat leo anatarajiwa kurejea kazini baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakufanya kosa lolote kuhusiana na mauaji ya kifo cha Mwanablogi na Mwalimu Albert Ojwang ambaye aliyefariki dunia katika mikononi mwa polisi.

Albert Ojwang

Bwn Ojwang alikamatwa na polisi nyumbani kwao Magharibi mwa Kenya na maafisa wa polisi waliodai alimtusi mkubwa wao na kupelekwa hadi katika kituo cha polisi jijini Nairobi ambapo aliripotiwa kupigwa hadi kufa.

Awali Naibu Mkuu wa Polisi Eliud Lagat, alishinikizwa na umma kujiulu kwa madai kuwa alihusika na kifo cha Bwn Ojwang, baada ya ujumbe wa Mwanablogi huyu kabla ya kifo chake kumhusisha na ufisadi.

Kifo cha Bw Ojwang kilisababisha maandamano ya wanaharakati nchini Kenya dhidi ya polisi na serikali, waandamanaji wakiilaani matukio ya mauaji na utekaji nyara wa raia, akiwemo Ojwang.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI