Rais wa Marekani Donald Trump aliwatunza wachezaji wa Chelsea Kombe na kushangilia nao jukwaani kufuatia ushindi wao wa fainali ya kombe la Dunia la Vilabu dhidi ya PSG mjini Newyork.
Trump alitakiwa kushuka jukwaani baada ya kukabidhi kombe lakini alisalia hapo, hali aliyowashangaza wachezaji wa Chelsea na watazamaji.
Mchezaji wa Chealsea Cole Palmer alisema '' ilikuwa hali ya kuchanganya kidogo' pale Trump aliposalia jukwaani huku mchezaji mwenzake Reece James akiongeza kusema '' nilitarajia ataondoka jukwaani ...lakini yaonekana hakutaka kufanya hivyo.''
Chelsea ulipata ushindi wa 3-0 dhidi ya PSG katika mchezo wa kuvutia na uliowastaajabisha wengi.
Wachambuzi wengi na mashabaki wa kamdanda waliitabiria PSG ushindi kutokana na rekodi yao ya ushindi na kusakata kandanda safi.
Hata hivyo Chelsea waliwaduwaza. Fainali hiyo pia ilifana kwa shamra shamra lukuki za nje ya uwanja na kuhudhuriwa na watu kadhaa mashuhuri wakiongozwa na Trump.
0 Comments