Header Ads Widget

MAPIGANO KATI YA THAILAND NA CAMBODIA YAINGIA SIKU YA TATU LICHA YA WITO WA KUSITISHA MAPIGANO

 


Cambodia imetoa wito wa kusitishwa "mara moja" kwa mapigano na Thailand, kwani nchi hizo mbili zimeshuhudia zaidi ya watu 32 wakiuawa, wakiwemo raia, katika mapigano yanayoendelea mpakani.

Balozi wa Cambodia katika Umoja wa Mataifa, Chhea Keo, alisema nchi yake iliomba mapatano "bila masharti", akiongeza kuwa Phnom Penh pia alitaka "suluhisho la amani la mzozo huo".

Thailand haijatoa maoni hadharani kuhusu pendekezo hilo, huku ikikataa upatanishi wa watu wengine. Hapo awali ilitangaza sheria ya kijeshi katika wilaya nane zinazopakana na Kambodia.

Mapigano kwenye mpaka wa Thailand na Kambodia yamendelea hadi siku ya tatu na mambo mapya yaliibuka siku ya Jumamosi huku pande zote mbili zikitafuta uungwaji mkono wa kidiplomasia, kila upande ukisema umejilinda na kuutaka upande mwingine usitishe mapigano na kuanza mazungumzo.

Takriban watu 32 wameuawa na zaidi ya watu 130,000 wamekimbia makazi yao katika mapigano mabaya zaidi kati ya majirani wa Kusini Mashariki mwa Asia katika kipindi cha miaka 13.

Watu wakwa wamepumzika ndani ya makazi ya muda katika jimbo la Srisaket, baada ya Thailand na Cambodia kufyatuliana risasi kali kwa siku ya pili siku ya Ijumaa huku mapigano ya mpakani yakizidi na kuenea, huku kiongozi wa Kambodia akisema Thailand imekubali pendekezo la Malaysia la kusitisha mapigano lakini ikarudi nyuma,

Jeshi la majini la Thailand lilisema kulikuwa na mapigano katika jimbo la pwani la Trat mapema Jumamosi, eneo jipya zaidi ya kilomita 100 (maili 60) kutoka maeneo mengine ya vita kwenye mpaka unaopiganiwa kwa muda mrefu.

Nchi hizo mbili zimekabiliana tangu kuuawa kwa mwanajeshi wa Cambodia mwishoni mwa mwezi Mei wakati wa mapigano mafupi.

Vikosi vya pande zote za mpaka viliimarishwa huku kukiwa na mzozo mkubwa wa kidiplomasia ambao umeitikisa serikali ya mseto dhaifu ya Thailand na kuifanya ikaribie kuanguka.

Idadi ya waliofariki Thailand imesalia 19 siku ya Jumamosi, huku msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Cambodia Maly Socheata akisema wanajeshi watano na raia wanane wameuawa katika mapigano hayo.

Katika wilaya ya Kanthralak katika mkoa wa Sisaket nchini Thailand, kwenye mpaka karibu na baadhi ya mapigano, mfanyakazi wa hoteli Chianuwat Thalalai alisema kuwa mji umeharibiwa.

Thailand na Kambodia zimezozana kwa miongo kadhaa juu ya mamlaka ya maeneo mbalimbali ambayo hayajawekewa mipaka kwenye mpaka wao wa ardhi wa kilomita 817 (maili 508), huku kukiwa na umiliki wa mahekalu ya kale ya Kihindu Ta Moan Thom na eneo la Preah Vihear lililojengwa karne ya ndio msingi wa mizozo huo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI