Header Ads Widget

MAGARI 50 YA SHULE YATIWA MBARONI MOROGORO, POLISI WASEMA “HATUTAONEA HAYA”

 


Na Mwandishi Wetu, Matukio Daima, Morogoro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linaendelea na ukaguzi wa magari yanayobeba wanafunzi, ambapo hadi kufikia Julai 9, jumla ya magari 50 yamezuiwa kuendelea na kazi hiyo baada ya kukutwa na kasoro mbalimbali za kiusalama zinazohitaji matengenezo ya haraka.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, akieleza kuwa jumla ya shule 90 zimefikiwa na magari 147 kukaguliwa tangu kuanza kwa zoezi hilo Juni 10 mwaka huu. 


Kati ya magari hayo, 97 yamekidhi vigezo na kuruhusiwa kuendelea kutoa huduma.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda Mkama amesema ukaguzi huo unatekelezwa na kikosi cha usalama barabarani kwa lengo la kulinda maisha ya wanafunzi, huku akiwataka madereva na wamiliki wa magari kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za usalama wa barabarani bila kukwepa majukumu yao.


“Tunaendelea na ukaguzi na hatutakuwa na muhali kwa yeyote atakayekiuka sheria. Lengo letu ni usalama wa watoto wetu,” amesema Kamanda Mkama.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI