Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametia saini mswada ambao wakosoaji wanasema unadhoofisha uhuru wa mashirika ya kupambana na ufisadi nchini humo, na kusababisha maandamano na kukosolewa kimataifa.
Wakosoaji wanasema sheria hiyo mpya inadhoofisha mamlaka ya Ofisi ya Kitaifa ya Kupambana na Ufisadi (Nabu) na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kupambana na Ufisadi (Sapo) – na kuziweka chini ya udhibiti wa mwendesha mashtaka mkuu.
Katika hotuba yake siku ya Jumatano, Zelensky alisema mashirika yote mawili bado "yatashirikiana kikazi", lakini yanahitaji kuondolewa dhana ya "ushawishi wa Urusi".
Baada ya mswada huo kupitishwa, mamia ya watu walikusanyika mjini Kyiv kwa maandamano makubwa zaidi dhidi ya serikali tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mnamo Februari 2022.
Maandamano pia yalionekana katika miji ya Lviv, Dnipro na Odesa.
"Tulichagua Ulaya, sio utawala wa mtu mmoja," lilisema bango lililoshikiliwa na mmoja wa waandamanaji. "Baba yangu hakufa kwa hili," mwingine alisema.
Mwendesha mashitaka mkuu wa Ukraine, ambaye ni mwaminifu kwa Zelensky, Ruslan Kravchenko, sasa ataweza kuidhinisha upya uchunguzi wa ufisadi kwa wachunguzi wanaoweza kuumiwa vibaya, na hata kuzifunga.
Katika hotuba yake, Zelensky alikosoa ufanisi wa miundombinu ya kupambana na ufisadi ya Ukraine, akisema kesi zimekuwa "zikichukua muda mrefu".
0 Comments