Rais wa zamani wa Colombia, Álvaro Uribe, amehukumiwa kwa kosa la kujaribu kushawishi mashahidi katika kesi ya ufisadi inayomkabili, hatua ambayo imeibua hisia mseto nchini humo na kuvuta hisia za kimataifa.
Hukumu hiyo imetolewa rasmi jana jijini Bogotá, baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa kwa kipindi cha takriban miezi sita na mamlaka za haki jinai nchini Colombia, ukihusisha ushahidi kutoka kwa mashahidi kadhaa pamoja na mawasiliano yaliyorekodiwa.
“Mahakama imejiridhisha kuwa mtuhumiwa alijaribu kwa njia zisizostahili kushawishi mashahidi ili wapotoshe ushahidi katika kesi ya awali iliyomkabili,” alisema Jaji Mkuu wa Mahakama ya Bogotá katika hukumu yake.
Uribe, ambaye alihudumu kama Rais wa Colombia kati ya mwaka 2002 hadi 2010, amekuwa akikanusha vikali tuhuma hizo, akizitaja kuwa ni njama za kisiasa dhidi yake. Hata hivyo, mahakama imebaini kuwepo kwa ushahidi wa kutosha unaoonyesha jitihada zake za kuvuruga mchakato wa haki.
0 Comments