Header Ads Widget

BETWAY MDHAMINI MKUU MPYA WA SIMBA SC KWA MIAKA MITATU



 Na Leonard Johnson 

Klabu ya Simba SC imeandika historia mpya kwa kutangaza rasmi kuingia kwenye mkataba mnono wa udhamini na kampuni kubwa ya michezo ya kubashiri, Betway. Mkataba huo una thamani ya shilingi bilioni 20 na utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu, ukifanya Betway kuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo maarufu Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa leo wakati WA uzinduzi huo wa mdhamini mpya, Betway sasa anachukua nafasi ya kampuni ya Mbet, ambaye alikuwa mdhamini wa awali wa Simba SC. Hatua hii inaonesha ukuaji mkubwa wa kibiashara kwa klabu hiyo, ambayo imekuwa ikijitahidi kuvutia wawekezaji na wadhamini wakubwa katika kipindi cha hivi karibuni.

Taarifa hii imepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Simba, wengi wakiona ni ishara njema ya maendeleo ya klabu yao kuelekea malengo ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na kushiriki kwa mafanikio kwenye michuano ya kimataifa kama CAF Champions League.

Kwa miaka mitatu ijayo, mashabiki wa Simba SC watashuhudia nembo ya Betway iking'aa kwenye jezi za timu hiyo, pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii na kibiashara zitakazokuwa zikifanyika chini ya udhamini huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI