Header Ads Widget

BALOZI SIRO ATAKA KASULU KUVUTIA WAWEKEZAJI WA VIWANDA

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Siro (mwenye suti) akitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mufindi Factory kilichopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima Media Kigoma 

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Siro ameuataka uongozi wa serikali wilaya ya Kasulu kuvutia wawekezaji na kuwalinda ili kutimiza azma ya serikali ya kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkakati kwa uchumi na biashara.

Balozi Siro alitoa kauli hiyo alipofanya ziara kutembelea kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mufindi Factory  ambacho kinaendelea kujengwa ambapo kukamilika kwake kutawezesha kuzalisha tani 100 za sukari kwa mwaka.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wilaya ya Kasulu ina maeneo makubwa na mazuri kwa ajili ya uwekezaji hasa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo hivyo lazima Halmashauri na mamlaka za serikali wilayani humo kuhakikisha wanavitangaza vivutio kwa ajili ya uwekezaji mkubwa lakini pia kuwalinda wawekezaji watakaojitokeza ili wafanya uwekezaji wao kuwa na  tija.

Katika ziara hiyo Balozi Siro alisema kuwa kiwand hicho ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi ya mkoa ikiwemo kutoa ajira, kusaidia upatikanaji wa uhakika wa sukari mkoani humo lakini pia kiwanda hicho kitazalisha umeme ambao pia utatumiwa na wananchi wa mkoa Kigoma.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa mkoa katika ziara hiyo, Meneja Uendeshaji wa kiwanda hicho, Saride Satyanarayana alisema kuwa wanatarajia ujenzi wa kiwanda hicho utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 117 utakapokamilika mwaka 2027 ambapo sukari itaanza kuzalishwa na kwamba tayari mashamba yenye ukubwa wa hekta 30,000 yameshaanza kupandwa miwa.

Satyanarayana alisema kuwa kiwanda kitakapoanza uzalishaji kitakuwa kinazalisha sukari tani 100,000 kwa mwaka, kitazalisha karatasi za kutengeneza fedha za noti lakini pia kitazalisha umeme ambao utaweza pia kutumika na wananchi wa kawaida na kwamba ajira za watu 500 zitatolewa.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI