Header Ads Widget

WAASWA KUWEKEZA KUEPUKA MSONGO WA MAWAZO.

 

Na Matukio Daima App, Mbeya.

Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) Kanda ya nyanda za juu kusini, umekutana na waandishi wa habari mkoa wa Mbeya na kueleza namna ambavyo mfuko huo wa hifadhi ya jamii kwa wastaafu unavyowasaidia wastaafu.

Meneja ya PSSSF kanda ya Nyanda za juu kusini Ramadhan Mgaya akizungumza na waandishi wa habari Juni 09, 2025 jijini Mbeya, amesema mfuko huo umeboresha huduma zake na unaendelea kuongeza wanachama wake ili kuwasaidia kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye baada ya kustaafu.

Mgaya amesema wastaafu wengi huwa na maisha magumu baada ya kazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutojiandaa na maisha ya kustaafu hasa kiuchumi na kosaikolojia hivyo mfuko huo upo kwa sababu ya kutojiandaa kwa maisha ya kustaafu.

Amesema ikiwa watajiandaa ikiwa ni pamoja na kujiunga na mfuko huo kwa wastaafu wa Umma pia watanufaika na fursa mbalimbali ikiwemo za kiuwekezaji, mikopo na kulipwa pensheni wao na wategemezi ambapo pia kwa mtu mmoja mmoja wasiokuwa watumishi wa umma wana fursa ya kipekee kupata nafasi ya kujiunga na vifurushi vyao kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Umma PSSSF.

Vicent Msola ni mstaafu ambaye alikuwa afisa maendeleo ya jamii hasa katika Halmashauri za Chunya na Mbeya jiji, anasema amenufaika kuwa mwanachama wa PSSSF kwani baada ya kustaafu hivi karibuni alianza kupata mafao yake ndani ya muda mfupi usiozidi miezi miwili hivyo kuwataka wastaafu watarajiwa kujiunga na mfuko huo ili kuepukana na matatizo yanayoepukika baada ya kustaafu ikiwemo msongo wa mawazo.

Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) kupitia makamu mwenyekiti wake Joseph Mwaisango na Mweka hazina bi. Rukia Chasanika, wameushukuru mfuko wa PSSSF kwa kuona haja ya kuketi na kundi la waandishi wa habari ili kuwapa elimu ya mfuko huo na namna unavyofanya kazi kwa watumishi wa Umma na jamii kwa ujumla na kuahidi wanahabari kuwa na ushirikiano na mfuko huo katika kuhakikisha unahudumia jamii yake ipasavyo.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI