Header Ads Widget

UWAMAKIZI YAGUSA MAISHA YA WAKULIMA KWA MICHE YA KAKAO NA KARAFUU

 


NA AMINA SAIDI,TANGA.

KATIKA kuendeleza juhudi za uhifadhi mazingira ya bonde la Zigi sambamba na kuinua kipato cha wananchi umoja wa wakulima wahifadhi mazingira Kihuhwi Zigi(UWAMAKIZI) umeendelea na zoezi la ugawaji wa miche ya miti ya biashfara kwa wakulima katika vijiji vya Wilaya ya Muheza na Korogwe.

Zoezi hilo ambalo lilifanyika katika vijiji vya Potwe Ndondondo,Potwe Mpirani, Kwemwewe,Sakale,(Muheza)na Ubiri(Korogwe)ukiwa ni sehemu ya maeneo ya juu Kidakio cha Zigi ambapo zaidi ya miche 36,000 ilisambazwa ikiwemo miche ya Karafuu,Kakao, Parachichi, miti ya mbao ambapo kijiji cha Sakale kilipokea miche 6000, Kwemwewe 14,000,Ubiri 800 na vijiji vya Potwe Mpirani na Potwe Ndondondo miche 16000 kwa pamoja.

Mradi huo unatekelezwa kwa uhifadhi wa TANGA UWASA na WATER FUND chini ya Nature Conservancy (TNC)na GIZ kwa lengo la kulinda vyanzo vya maji kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kuinua uchumi wa jamii za wakulima.

Akizungumza wakati wa tukio hilo Meneja wa Tanga UWASA Kanda ya Muheza ambaye pia ni msimamizi Mkuu wa shughuli za mazingira Ramadhan Nyambuka Alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa miche hiyo ili kuhakikisha inakua na kuleta tija.

Aidha alitoa wito kwa wakulima kuendeleza kuonyesha moyo wa uzalendo na uwajibikaji kwa mazingira yajayo.

Kwa upande wake Mratibu wa mfuko wa maji Tanga (WATER FUND)Alex Njahani alieleza kufurahishwa na mwitikio mkubwa wa wakulima ambapo alisema kuwa hamasa hiyo ni kiashiria tosha cha mabadiliko ya fikra na utayariwa jamii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira.

Naye Mwenyekiti wa wa kijiji cha Sakale Alen John Giza alitoa shukrani kwa UWAMAKIZI na wadau wake kwa kuwaletea mradi wenye manufaa makubwa huku akiahidi kushirikiana na wanakijiji kusimamia kikamilifu upandaji na utunzaji wa miche iliyotolewa. 

Awali akizumngumza  Mwenyekiti wa UWAMAKIZI,Twaha Mbaruku alieleza kuwa zoezi hilo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuimarisha juhudi za uhifadhi wa  mazingira katika maeneo ya juu ya bonde la Zigi.

Alisisitiza kuwa kupitia ushirikiano na wadau wa maendeleo kama Tanga UWASA, WATER FUND,TNC na GIZ, UWAMAKIZI inalenga kuwajengea wakulima uwezo wakulinda mazingira na kuinua vipato vyao kupitia kilimo cha miti ya biashara .

Mbarouk aliongeza kuwa zoezi hilo linawapa mwitiko mkubwa  na kuwavutia kutoka kwa watu wa rika zote, kwani ni lilionyesha mshikamano na ari ya pamoja katika kutunza mazingira .

Hata hivyo wananchi walijitokeza kwa wingi kwaajili ya kupata miche iyotolewa akiwepo na msanii maarufu alyejulikanana ka jina laPwepwe Lee jina halisi Hassan  ambaye alipata nafsi ya kuzungumza na kusema licha ya kujihusisha  na Sanaa ya burudani na mdau wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira  pia anajihusisha nakilimo.

"Kupokea miche hii ni sehemu ya kuboresha shamba langu,kama msanii na mwanajamii ninaamini ni muhimu kuonyesha mfano kwa  vitendo si kwa maneno peeke"alisema kwa kujiamini.

Zoezi hili limthibitisha kuwa ushirikiano katika jamii,Taasisi za ndani na wadau wa Kimataifa unaweza kuleta mabadiliko chanya si tu katika uhifadhi wa Mazingira bali pia katika ustawi wa kiuchumi wa Wananchi. 

Mwisho.




SIMULIZI CHINI ⬇️⬇️⬇️


Ndoa yangu ilikaribia kuvunjika, hivi ndivyo nilivyoiokoa! 

Jina langu ni Anna, na miezi michache iliyopita, mimi na mume wangu tulikaribia kutengana. Iliniogopesha sana kwa sababu nilimpenda sana. Tulikuwa pamoja kwa miaka 15, hivyo tulikuwa tumejenga maisha pamoja na kujaliwa watoto wawili. 

Ndoa yetu ilikumbana na hali mbaya iliyojaa mabishano, kutoaminiana na hata kudhulumiwa kihisia. Mume wangu alikasirika kila wakati na kugombana hata kwa jambo dogo mbele ya watoto. Hakutaka kuwa karibu nami hali iliyoniumiza sana. 

Siku moja alirudi nyumbani na akatangaza kuwa anaondoka. Alisema hanipendi tena, hivyo anataka kunipa talaka. Nilivunjika moyo. Sikuamini kuwa ndoa yetu inaenda kuvunjika kwa urahisi kiasi hicho. 

Nilimpigia simu mama yangu na kumueleza jambo hilo. Mama alinishauri niwasiliane na Kiwanga Doctors ambao walikuwa wamemsaidia katika hali kama hiyo kipindi cha nyuma.

Alisema wanaweza kukomesha talaka mara moja. Nilipata namba zao na kuwapigia mara moja ikiwa ni baada ya mume wangu kuondoka.

Siku iliyofuata, nilifika kwa Kiwanga Doctors huko Migori, Kenya, huko punde tu walifanya uchawi wa kuokoa ndoa yangu na mwingine wa kurudisha penzi la mume wangu kwangu kama ilivyokuwa hapo awali kipindi ambacho tunaoana. 

Kusema kweli nilihisi kama miujiza maana jioni hiyo tu, mume wangu alirudi nyumbani, huku akiniomba msamaha mimi na watoto kwa kuwa mbali nasi bila kujali lolote kuhusu familia yake ambayo inamtegemea. 

Usiku huo, tuliungana tena kwa njia ambayo hatukuwa nayo kwa muda mrefu. Sasa, mume wangu ananipenda zaidi kuliko hapo awali, na ninawashukuru sana Kiwanga Doctors kwa kuokoa ndoa yetu.

Ikiwa unapitia kitu kama hicho, ninakushauri kuwa fika au wasiliana na Kiwanga Doctors. Tiba zao zinafanya kazi haraka na wanaweza kukusaidia katika changamoto mbalimbali za kimaisha, kuanzia masuala ya uhusiano hadi matatizo ya kiafya. 

Ni watu wengi hadi sasa wamepata mafanikio, uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba  +255 763 926 750  au tembelea tovuti yao, maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI