Na Shemsa Mussa -Matukio daima
Kagera.
Ujenzi wa daraja la kyetema lililopo katika Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera linatalajiwa kukamilika mnamo Mwezi Novemba 2025.
Meneja wa Tanroad Mkoa wa Kagera Eng Ntuli Mwaikokesya ameeleza namna ujenzi huo unavyoendelea na kusema kuwa Mkandarasi aliyepewa jukumu Hilo la ujenzi anaendelea vizuri licha ya kuwepo kwa changamoto ya mvua katika eneo Hilo.
Katika kuhakikisha shughuli hiyo haikwamishwi na changamoto yoyote Eng Ntuli amesema limewekwa daraja mbadala kwa ajili ya matumizi mengine ikiwa Barabara hiyo ndio inatumiwa na Magari yote yaendayo Mikoani na nchi jirani.
"Wakati Mkandarasi anaendelea na ujenzi wa daraja bado wakati huo huo anaiangalia hii njia au Barabara mbadala tuliyoiweka ili isewe changamoto au kikwazo kwa watumiaji wote na tunafahamu hii Barabara ndio pekee inayotumika kwa magari yote yaendayo Mikoani hata nchi jirani hivyo tupo makini sana katika Hilo,amesema Eng Ntuli "
Amesema Ujenzi wa dalaja Hilo la kyetema utaghalimu kiasi Cha Shilingi Billion 8.5 mpaka kukamilika kwake amesema kwa kipindi Cha ujenzi huo wananchi na watumiaji wa Barabara hiyo wataendelea kufanya shughuli zao bila kuwa na changamoto huku wao kama Tanroad wakiendelea kusimamia ujenzi huo kukamilika kwa wakati
Aidha Eng Ntuli ameeleza ujenzi wa Barabara wa njia Nne pamoja na daraja la kanoni ndani ya manispaa ya Bukoba Mkoani humo huku akisema Barabara hiyo yenye vipande viwili kipande Cha kwanza kikitokea rwamishenye Hadi hamgembe na hamgembe mpaka stendi ikiunganishwa na dalaja la kanoni,amesema kwa Sasa wanaendelea na ujenzi wa dalaja wakiwa wanasubilia msimu wa mvua kuisha ili waendelea na ujenzi wa Barabara hiyo
"Kwa kipindi chote Cha mvua tulikuwa tunaendelea na ujenzi wa dalaja kwa sababu kwenye mvua huwezi kufanya ujenzi wa Barabara hivyo tu Niwaombe wananchi tuwe na subira naamini kwa sababu mvua ndio zinaishilia basi tutaanza kwa kurekebisha maeneo yote ambayo yameadhiliwa na mvua huku kazi nyingine za ujenzi zikiendelea, ameongeza Eng Ntuli"
Pia ametoa Rai kwa madereva na watumiaji wa wa Barabara kuhakikisha wanafuata sheria pamoja na maelekezo ya Barabarani ambayo yanatolewa na kuhakikisha kwa kipindi hiki Cha ujenzi wa miundombinu hiyo hawapiti kwenye Barabara walizozuiliwa.
0 Comments