Header Ads Widget

TUNAKUPONGEZA MAMA KWA ZIARA YENYE MATUMAINI SIMIYU WATANZANIA ANATUDAI KUTIKI OKTOBA – AIDAN MLAWA

 


Na Matukio Daima Media

PAMOJA na wananchi wa Mkoa wa Simiyu kupongeza Ziara ya Rais mkoani humo pia mdau wa maendeleo nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Aidan Mlawa, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa ziara yake muhimu na yenye matumaini katika Mkoa wa Simiyu.

Mlawa amesema kuwa ziara hiyo imekuwa ya kihistoria na yenye mguso wa moja kwa moja kwa wananchi, kwani imeonyesha wazi dhamira ya dhati ya Rais Samia ya kuwasikiliza wananchi na kuwaletea maendeleo ya kweli.

Akizungumza na Matukio Daima Media, Mlawa alisema ziara hiyo imeonesha namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita iko makini katika kuhakikisha kila kona ya nchi inapata huduma bora za kijamii na kiuchumi.

"Kupitia ziara hii, Mama yetu Samia amethibitisha kwamba Mkoa wa Simiyu si wa kusahaulika, bali ni sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa letu. 

Hatua na miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ni ushahidi wa uongozi wenye maono na usikivu," alisema Mlawa.

Katika kuonesha matokeo ya uongozi wa Rais Samia, Mlawa alitaja baadhi ya miradi mikubwa ya kimkakati ambayo imeleta mwanga mpya kwa wananchi wa Simiyu, ikiwemo:

Hospitali ya kisasa inayohudumia mikoa jirani, ikiwa na wodi, ICU, maabara na vifaa vya kisasa vya tiba.

Mradi mkubwa unaolenga kupunguza adha ya maji safi kwa wakazi wa Bariadi na maeneo jirani.

Ujenzi wa zaidi ya madarasa 300 ili kuongeza fursa ya elimu bora kwa watoto wa Simiyu.

Barabara ya kiwango cha lami inayorahisisha usafiri na uchumi wa ndani ya mkoa.

Ujenzi na ukarabati wa zaidi ya vituo 50 vya kutolea huduma za afya Kituo cha Biashara cha Mifugo na Mazao – Nyakabindi (Maswa)

Kitovu cha biashara kinachochochea uchumi wa wafugaji na wakulima,Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)

Kituo cha kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana ili kujiajiri na kuinua uchumi wa eneo,

Kuunganishwa kwa vijiji vingi na umeme kupitia REA Awamu ya Tatu.

Mlawa, ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na anayefahamika kwa mchango wake katika miradi ya kijamii na kusaidia watu wenye uhitaji, alisema kuwa ziara hiyo imechochea matumaini mapya kwa wananchi wa Simiyu.

Alisema serikali ya awamu ya sita imekuwa ikifanya kazi kubwa na kutekeleza miradi hiyo si tu mkoani Simiyu bali kila kona ya Tanzania ukiwemo mkoa wa Iringa na wilaya yake ya Kilolo ambako kazi kama hizo zimefanyika hivyo wana Kilolo hawana dani na Rais Samia Oktoba wanangoja kumlipa kwa kutiki CCM.

 "Kwa dhati kabisa tunasema: Asante Mama Samia kwa moyo wako wa huruma, uwajibikaji na maono makubwa ya kuijenga Tanzania mpya. Simiyu sasa ina matumaini, na wananchi wake wanajiona kusikika na kupewa kipaumbele," aliongeza Mlawa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI