Header Ads Widget

TRUMP ALIIAMBIA ISRAEL ISIMUUE KIONGOZI MKUU WA IRAN - RIPOTI

 

Rais wa Marekani Donald Trump amekataa mpango wa Israel wa kumuua Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, maafisa watatu wa Marekani wameambia mshirika wa BBC wa Marekani CBS News.

Trump aliripotiwa kumwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba kumuua Khamenei "si wazo zuri", kulingana na afisa mmoja. Rais hajatoa maoni yake hadharani kuhusu ripoti hiyo.

Mazungumzo hayo yanasemekana kutokea tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi yake dhidi ya Iran siku ya Ijumaa.

Wakati wa mahojiano na Fox News, Netanyahu hakuthibitisha moja kwa moja au kukanusha ripoti kutoka kwa Reuters kwamba Trump alipinga mpango wa kumuua ayatollah.

"Kuna ripoti nyingi za uongo za mazungumzo ambazo hazijawahi kutokea na sitaingia katika hilo," waziri mkuu wa Israel alisema.

"Lakini naweza kukwambia nadhani tunafanya kile tunachohitaji kufanya. Tutafanya kile tunachohitaji kufanya na nadhani Marekani inajua kipi ni kizuri kwa Marekani na sitazungumzia hilo zaidi."

Afisa wa Israel aliiambia CBS News kwamba "kimsingi" Israel haiwaui viongozi wa kisiasa, tunaangazia nyuklia na jeshi. Sidhani yeyote anayefanya maamuzi kuhusu programu hizo anapaswa kuishi kwa uhuru na urahisi".

Israel ilianzisha kwa mara ya kwanza mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nyuklia ya Iran na malengo mengine siku ya Ijumaa. Nchi hizo mbili zimeendelea kufanya mashambulizi makubwa kati yao tangu wakati huo, na mashambulizi yakiingia siku ya tatu Jumapili.

Katika chapisho lake la hivi karibuni kuhusu hali ilivyo Mashariki ya Kati, Trump alisema "Iran na Israel zinapaswa kufanya mapatano", akiongeza kwamba atawafanya wawili hao wasitishe uhasama "kama vile ilivyotokea kwa India na Pakistan" akimaanisha makabiliano ya hivi karibuni kati ya nchi hizo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI