Header Ads Widget

TICD TENGERU YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

 

Katika kuunga mikono juhudi za serikali ya awamu ya sita Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD imeadhimisha Siku ya Mazingira Dunia Juni 5 mwaka huu kwa kufanya Kongamano la uwasilishwaji wa tafiti zitakazosaidi kupunguza matumizi ya plastiki na kutunza mazingira.

Akizungumza katika Kongamano hilo ambalo limafanyika katika chuo hicho Mkuu wa chuo hicho Dkt.Bakari George amesema hatua hiyo ni uungaji mkono juhudi za Rais Dkt. Samia ambaye amekuwa akihimiza agenda mbalimbali katika utunzaji wa mazingira ikiwemo mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ,ajenda inayoboresha mifumo ya upishi kwa kutumia nishati safi na salama kwa mazingira pamoja na uimarishaji wa uchumi wa kijani na matumizi ya Teknolojia rafiki kwa mazingira.

Aidha amesema kama Taasisi ya Elimu ya juu inayozalisha wataalamu wa maendeleo ya jamii imeendelea kuonyesha dhamira ya dhati katika kutunza mazingira kwa kutekeleza kwa vitendo jambo hilo ikiwemo utoaji wa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kupitia program mbalimbali zinazojumuisha vipengele vya mazingira kwa wanafunzi wa ngazi ya cheti hadi shahada za uzamili.


Vilevile amewataka wanataaluma na jamii kwa ujumla kufahamu kuwa mazingira si jambo la hiari bali ni jukumu la pamoja ambapo Imani yake kubwa kupitia tafiti,elimu na ushirikiano wa pamoja wataweza kupunguza matumizi ya plastiki zisizoharibika na kuhamasisha matumizi ya nishati safi kama sehemu ya ajenda ya kukuza ubunifu wa vijana kwenye urejelezaji wa taka na kuwa msingi thabiti wa maendeleo endelevu.

Akifungua Kongamano la uwasiliahwaji wa tafiti mbalimbali za kuzuia uchaguzi wa mazingira lililofanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru TICD,kwenye Kilele cha Maadhimisho  ya Siku ya Mazingira Duniani,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amir Mkalipa amesema ofisi yake kwa kushirikiana na mashirika ya kijamii, taasisi za elimu na sekta binafsi zimeweka juhudi za kupambana na uchafuzi wa plastiki kuwa ni mojawapo ya agenda ya kudumu.

Aidha amesema kupitia ushirikiano huo wametekeleza mambo mbalimbali ikiwemo yanzishwaji wa vituo vya kuchakata taka katika maeneo ya Ngaramtoni, Usa river, King'ori Wilayani Arumeru vinavyotumika kama mfano wa usimamizi wa taka za plastiki ambapo pia amesema program ya Shule rafiki wa Mazingira inayotekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi zisizo za kiserikali imewaelimisha watoto kuhusu uchafuzi wa plastiki na na kuwaelimisha kumchukuwa hatua ni juhudi za Wilaya ya Arumeru katika kupambana na changamoto hiyo.

Mkalipa amesema serikali imeendelea kutekeleza mikakati wa madhubuti ikiwemo marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki ya mwaka 2019 ,Tanzania ikiwa ni mojawapo ya nchi za kwanza Afrika Mashariki kutekeleza sera hiyo kwa ufanisi na kusema kuwa serikali ya awamu ya sita imeandaa mkakati wa Taiga wa Usimamizi wa taka wa mwaka 2022 hadi 2027 unaosisitiza urejeleaji wa taka ,udhibiti wa taka za plastiki na matumizi mbadala ya bidhaa zisizo na madhara ambapo mpango huo umelenga kudhibiti athari za hewa ukaa na na kuhamasisha uchumi wa kijani.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI